If this scheme pleases you, click here to download.
WK | KIPINDI | MADA KUU | MADA NDOGO | SHABAHA | SHUGHULI ZA UFUNZAJI | MASWALI DADISI | NYENZO | TATHMINI | MAONI |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
2 | 1 |
UTUNZAJI WA WANYAMA
Kusikiliza na Kuzungumza |
Semi - Tashbihi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya tashbihi ili kuipambanua na tungo zingine. Kutambua tashbihi katika matini ya fasihi simulizi. Kueleza matumizi ya tashbihi katika matini ya fasihi simulizi. Kuchangamkia matumizi ya tashbihi katika tungo za fasihi simulizi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kueleza maana ya tashbihi. Kutambua tashbihi kama "mrefu kama twiga", "maridadi kama tausi" katika tungo simulizi. Kueleza matumizi ya tashbihi katika tungo za fasihi simulizi. Kushiriki katika uwasilishaji wa tashbihi. |
Je, tunatumia mbinu gani za lugha katika kuwasilisha tungo za fasihi simulizi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 24
Kadi za tashbihi Vifaa vya kidijitali Matini ya mwalimu |
Kutambua tashbihi katika tungo za fasihi simulizi
Kueleza matumizi ya tashbihi
Kutunga tashbihi
Kutofautisha tashbihi na semi zingine
|
|
2 | 2 |
Kusikiliza na Kuzungumza
|
Semi - Sitiari
Semi - Methali |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya sitiari ili kuipambanua na tungo zingine. Kutambua sitiari katika matini ya fasihi simulizi. Kueleza matumizi ya sitiari katika matini ya fasihi simulizi. Kuchangamkia matumizi ya sitiari katika tungo za fasihi simulizi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kueleza maana ya sitiari. Kutambua sitiari kama "Yeye ni twiga", "Yeye ni simba" kutoka kwenye tungo simulizi au kifaa cha kidijitali. Kueleza matumizi ya sitiari katika tungo za fasihi simulizi. Kushiriki katika uwasilishaji wa sitiari. |
Kwa nini tunatumia sitiari kuwasilisha tungo za fasihi simulizi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 25-27
Matini zilizo na sitiari Chati za sitiari Vifaa vya kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili uk. 27-29 Orodha ya methali Matini ya mwalimu |
Kutambua sitiari katika tungo za fasihi simulizi
Kueleza matumizi ya sitiari
Kutunga sitiari
Kutofautisha sitiari na tashbihi
|
|
2 | 3 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya shairi ili kulitofautisha na tungo zingine. Kujadili sifa za ushairi kama utanzu wa fasihi andishi. Kueleza sifa za ushairi katika shairi. Kufurahia kuchambua ushairi kama utungo wa fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutafiti maana ya shairi vitabuni au mtandaoni ili kulitofautisha na tungo nyingine. Kujadili na wenzake sifa za ushairi kama utanzu wa fasihi andishi. Kusoma mashairi katika diwani iliyoteuliwa na mwalimu na kueleza sifa za ushairi katika mashairi hayo. Kuwasomea wenzake sifa alizotambua katika mashairi aliyoyasoma ili wamtolee maoni. |
Je, shairi ulilowahi kusoma lilikuwa linazungumzia nini?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 30-31
Diwani ya mashairi iliyoteuliwa Vifaa vya kidijitali Matini ya mwalimu |
Kutambua sifa za ushairi
Kusoma shairi kwa kuzingatia vipengele vyake
Kuandika muhtasari wa sifa za ushairi
Kujadili ujumbe wa shairi
|
|
2 | 4 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya shairi ili kulitofautisha na tungo zingine. Kujadili sifa za ushairi kama utanzu wa fasihi andishi. Kueleza sifa za ushairi katika shairi. Kufurahia kuchambua ushairi kama utungo wa fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma shairi "Wanyama tuwalindeni, waishi pasi nakama" katika diwani iliyoteuliwa na mwalimu. Kutambua vipengele vya shairi kama vile vina, mizani, mishororo, kituo, na kadhalika. Kujadili na wenzake sifa za shairi alilolisoma. Kuwasomea wenzake shairi hilo kwa kuzingatia kanuni za usomaji wa mashairi. |
Je, unavutiwa na nini unaposoma shairi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 31-32
Diwani ya mashairi iliyoteuliwa Chati ya sifa za ushairi Vifaa vya kidijitali |
Kutambua sifa za ushairi katika shairi
Kusoma shairi kwa ufasaha
Kujibu maswali kuhusu shairi
Kufanya tathmini ya ujumbe wa shairi
|
|
3 | 1 |
Kuandika
|
Insha za Kubuni - Masimulizi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vipengele vya kufafanulia ujumbe wa insha ya masimulizi. Kufafanua ujumbe wa insha ya masimulizi kupitia kwa utangulizi, kiini na hitimisho. Kufafanua ujumbe wa insha ya masimulizi kupitia kwa wahusika. Kuandika insha ya masimulizi kwa kuzingatia ujumbe na muundo ufaao. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua vipengele vya kufafanulia ujumbe wa simulizi. Kusoma kielelezo cha insha ya masimulizi na kufafanua ujumbe kupitia kwa utangulizi, kiini na hitimisho. Kusoma kielelezo cha insha ya masimulizi kwenye matini za aina mbalimbali na kufafanua ujumbe kupitia kwa wahusika. Kujadili vigezo vya kutathmini insha ya masimulizi. |
Je, unafanya nini unaposimulia jambo ili ujumbe wako upate kueleweka zaidi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 33-34
Mifano ya insha za masimulizi Picha Vifaa vya kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili uk. 35 Matini ya mwalimu |
Kutambua vipengele vya insha ya masimulizi
Kufafanua ujumbe wa insha kupitia utangulizi, kiini na hitimisho
Kuandika mwongozo wa kutunga insha ya masimulizi
|
|
3 | 2 |
Sarufi
|
Vihusishi Vilinganishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vihusishi vilinganishi katika matini. Kutumia vihusishi vilinganishi ipasavyo katika matini. Kuchangamkia matumizi yafaayo ya vihusishi vilinganishi katika mawasiliano ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua vihusishi vilinganishi kama "kama", "sawa na", "mithili ya", "kupita", "kuliko" n.k. Kutambua vihusishi vilinganishi katika sentensi kama "Sungura alimchekelea Kobe na kumwambia, 'mimi ni mwepesi kuliko wewe.'" Kujaza nafasi katika sentensi kwa kutumia vihusishi vilinganishi. Kutunga sentensi akitumia vihusishi vilinganishi akizingatia utunzaji wa wanyama. |
Je, vihusishi vilinganishi na kihusishi 'na' huchangia vipi katika mawasiliano?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 36-37
Kadi za vihusishi vilinganishi Chati Vifaa vya kidijitali |
Kutambua vihusishi vilinganishi katika sentensi
Kujaza pengo kwa vihusishi vilinganishi
Kutunga sentensi zenye vihusishi vilinganishi
Kufanyiana tathmini
|
|
3 | 3 |
Sarufi
|
Kihusishi 'na'
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua kihusishi 'na' katika matini. Kutumia kihusishi 'na' ipasavyo katika matini. Kuchangamkia kutumia kihusishi 'na' katika mawasiliano ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua kihusishi 'na' katika sentensi kama "Waliwaona simba wakifukuzana na swara." Kutambua kihusishi 'na' katika sentensi kwa kukipigia mstari. Kujaza pengo kwa kutumia kihusishi 'na' panapohitajika. Kutunga sentensi na vifungu kwa kutumia kihusishi 'na' ipasavyo kuhusu utunzaji wa wanyama. |
Je, kihusishi 'na' kinatofautianaje na vihusishi vingine?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 37-38
Kadi za sentensi zenye kihusishi 'na' Vifaa vya kidijitali Matini ya mwalimu |
Kutambua kihusishi 'na' katika sentensi
Kutunga sentensi zenye kihusishi 'na'
Kujaza pengo kwa kihusishi 'na'
Kufanyiana tathmini
|
|
3 | 4 |
UTUNZAJI WA MALIASILI
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Semi - Vitendawili
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya vitendawili; Kutambua vipengele vya uwasilishaji wa vitendawili; Kutambua vitendawili katika matini; Kuwasilisha vitendawili kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji wake; Kuchangamkia matumizi ya vitendawili katika tungo za fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutumia kamusi au mtandao salama kutafuta maana ya vitendawili; Kueleza maana ya vitendawili; Kutoa mfano wa kitendawili kutokana na maana aliyopata; Kutambua vipengele vya uwasilishaji wa vitendawili. |
Unazingatia nini unapowasilisha vitendawili?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 40
Kamusi Mtandao salama Kadi maneno KLB Top Scholar Kiswahili uk. 41 Picha Vifaa vya kidijitali |
Kutambua vitendawili;
Kueleza maana ya vitendawili;
Kuwasilisha vitendawili kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji
|
|
4 | 1 |
Kusikiliza na Kuzungumza
|
Semi - Nahau
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya nahau; Kutambua nahau katika matini; Kueleza maana za nahau; Kutumia nahau ipasavyo katika mawasiliano; Kuchangamkia matumizi ya nahau katika tungo za fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutumia kamusi au mtandao salama kutafuta maana ya nahau; Kueleza maana ya nahau; Kutoa mfano wa nahau kutokana na maana aliyopata; Jadili maana za nahau mbalimbali. |
Nahau hutumiwa kwa nini katika mawasiliano?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 42
Kamusi Mtandao salama Kadi za nahau |
Kutambua nahau;
Kueleza maana za nahau;
Kutumia nahau ipasavyo katika sentensi
|
|
4 | 2 |
Kusikiliza na Kuzungumza
|
Semi - Nahau
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua umuhimu wa nahau katika fasihi simulizi; Kueleza umuhimu wa nahau katika fasihi simulizi; Kutumia nahau ipasavyo katika mawasiliano; Kuchangamkia matumizi ya nahau katika tungo za fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusikiliza hadithi ya mwalimu iliyo na nahau; Kutambua nahau katika hadithi iliyosikilizwa; Kueleza maana za nahau zilizotambuliwa; Jadili umuhimu wa nahau zilizotambuliwa. |
Nahau huongeza ladha gani katika lugha?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 43
Hadithi ya sungura Kadi za nahau |
Kutambua nahau;
Kueleza umuhimu wa nahau;
Kutumia nahau ipasavyo
|
|
4 | 3 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Ufasaha
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha; Kueleza vipengele vya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha; Kusoma kifungu cha nathari akizingatia matamshi bora; Kusoma kifungu cha nathari akizingatia kasi ifaayo; Kujenga mazoea ya kusoma kwa ufasaha ili kufanikisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusikiliza na kumtazama mwalimu akisoma kifungu; Kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha; Kueleza vipengele alivyotambua kwa kuzingatia ubora wa matamshi, kasi ya usomaji, kiwango cha sauti na kuambatanisha ishara zifaazo. |
Unazingatia mambo gani unaposoma kwa ufasaha?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 44
Kifungu cha nathari Vifaa vya kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili uk. 45 Saa ya kidijitali |
Kutambua vipengele vya kusoma kwa ufasaha;
Kusoma kwa kuzingatia matamshi bora;
Kusoma kwa kasi ifaayo
|
|
4 | 4 |
Kuandika
|
Insha za Kubuni - Masimulizi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya lugha ya kitamathali; Kutambua lugha ya kitamathali katika insha ya masimulizi; Kujadili lugha ya kitamathali katika insha ya masimulizi; Kutumia lugha ya kitamathali katika insha ya masimulizi; Kufurahia matumizi ya lugha ya kitamathali katika kuandika insha. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutumia kamusi au mtandao salama kutafuta maana ya tamathali; Kueleza maana ya lugha ya kitamathali; Kutoa mifano ya tamathali za usemi; Kusoma insha ya masimulizi na kutambua lugha ya kitamathali iliyotumika. |
Lugha ya kitamathali huongeza ladha gani katika insha?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 47
Kamusi Mtandao salama Insha ya mfano |
Kueleza maana ya lugha ya kitamathali;
Kutambua lugha ya kitamathali katika insha;
Kutumia lugha ya kitamathali katika sentensi
|
|
5 | 1 |
Kuandika
|
Insha za Kubuni - Masimulizi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua wahusika katika insha ya masimulizi; Kujadili matendo ya wahusika katika insha ya masimulizi; Kujadili mandhari katika insha ya masimulizi; Kuandika insha ya masimulizi akizingatia lugha ya kitamathali, matendo ya wahusika na mandhari; Kufurahia kuandika insha za masimulizi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutafuta maana ya wahusika; Kusoma insha ya masimulizi; Kutambua wahusika katika insha ya masimulizi; Jadili matendo ya wahusika; Jadili mandhari katika insha aliyosoma. |
Unazingatia vipengele vipi unapoandika insha ya masimulizi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 48
Insha ya mfano Picha Vifaa vya kidijitali |
Kutambua wahusika katika insha;
Kujadili matendo ya wahusika;
Kujadili mandhari katika insha
|
|
5 | 2 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni - Masimulizi
Nyakati na Hali - -ki- ya masharti |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kuandika insha ya masimulizi akizingatia lugha ya kitamathali, matendo ya wahusika na mandhari; Kufanya marekebisho ya insha ya masimulizi; Kufurahia kuandika insha za masimulizi akizingatia lugha ya kitamathali, matendo ya wahusika na uchoraji wa mandhari. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kuandika insha akisimulia yaliyotokea katika siku ya upandaji wa miti; Kushirikiana na wenzake kusahihisha insha aliyoandika; Kuandika nakala safi ya insha baada ya kuirekebisha; Kuwasomea wenzake nakala safi ya insha aliyoandika. |
Kwa nini uchoraji wa mandhari ni muhimu katika insha ya masimulizi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 49
Orodha ya tathmini Karatasi za kuandikia KLB Top Scholar Kiswahili uk. 50 Chati Matini yenye sentensi za -ki- ya masharti |
Kuandika insha ya masimulizi;
Kutumia lugha ya kitamathali;
Kubainisha wahusika;
Kuchora mandhari
|
|
5 | 3 |
Sarufi
|
Nyakati na Hali - -ki- ya masharti
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua -ki- ya masharti katika matini; Kutumia -ki- ya masharti ipasavyo katika matini; Kujenga mazoea ya kutumia ipasavyo -ki- ya masharti ili kufanikisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kuteua sentensi zenye -ki- ya masharti; Kubadilisha sentensi ambazo hazina -ki- ya masharti ziwe na -ki- ya masharti; Kutunga sentensi tano akitumia -ki- ya masharti. |
Je, ni tofauti gani kati ya -ki- ya masharti na -ki- ya wakati?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 51
Karatasi zenye sentensi Vifaa vya kidijitali |
Kubadilisha sentensi ziwe na -ki- ya masharti;
Kutunga sentensi akitumia -ki- ya masharti;
Kufanya tathmini
|
|
5 | 4 |
Sarufi
|
Nyakati na Hali - -ka- ya kufuatana kwa vitendo
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua -ka- ya kufuatana kwa vitendo katika matini; Kueleza matumizi ya -ka- ya kufuatana kwa vitendo; Kutumia -ka- ya kufuatana kwa vitendo ipasavyo katika matini; Kujenga mazoea ya kutumia ipasavyo -ka- ya kufuatana kwa vitendo ili kufanikisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma sentensi zenye -ka- ya kufuatana kwa vitendo; Kutambua sentensi zenye -ka- ya kufuatana kwa vitendo; Kutunga sentensi akitumia -ka- ya kufuatana kwa vitendo; Kusomea mwenzake sentensi alizozitunga. |
-ka- ya kufuatana kwa vitendo hutumiwa wakati gani katika sentensi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 51
Karatasi zenye sentensi Kadi za maneno |
Kutambua -ka- ya kufuatana kwa vitendo;
Kutunga sentensi akitumia -ka- ya kufuatana kwa vitendo;
Kufanya tathmini
|
|
6 | 1 |
HUDUMA KATIKA ASASI ZA KIJAMII
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kusikiliza kwa Kutathmini
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini; Kubainisha vipengele vya kusikiliza kwa kutathmini; Kusikiliza na kutathmini ujumbe wa matini; Kuchangamkia kusikiliza kwa kutathmini ili kukuza stadi ya kusikiliza. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutazama picha ya vituo vya huduma na kueleza shughuli zinazotendeka; Kusikiliza mazungumzo katika kifaa cha kidijitali; Kutambua vipengele vya kusikiliza kwa kutathmini; Kujadili vipengele vya kutathmini katika mazungumzo aliyosikiliza. |
Unazingatia nini kutambua ikiwa mzungumzaji anasema ukweli?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 75
Picha Kifaa cha kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili uk. 76 Mazungumzo kwenye kifaa cha kidijitali |
Kubainisha vipengele vya kusikiliza kwa kutathmini;
Kutambua vipengele vya kusikiliza kwa kutathmini;
Kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini
|
|
6 | 2 |
Kusoma
|
Ufupisho
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya ufupisho; Kulinganisha kifungu asilia na ufupisho wake; Kubainisha vipengele vya ufupisho; Kufupisha kifungu kwa kuzingatia vipengele vya ufupisho; Kuchangamkia kusoma na kufupisha vifungu mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kulinganisha sentensi ndefu na fupi zenye ujumbe sawa; Kusoma vifungu A na B na kueleza kifungu kinachotoa habari kwa ufupi; Kubainisha vipengele vya ufupisho kwa kulinganisha kifungu A na B. |
Je, tunapofupisha kifungu tunasema ya muhimu tu?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 78
Vifungu vya ufahamu Kifaa cha kidijitali |
Kueleza maana ya ufupisho;
Kulinganisha kifungu asilia na ufupisho wake;
Kufanya tathmini
|
|
6 | 3 |
Kusoma
|
Ufupisho
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vipengele vya ufupisho; Kufupisha kifungu kwa idadi maalum ya maneno; Kuchangamkia kufupisha vifungu kwa mpangilio ufaao; Kuheshimu maagizo ya ufupisho. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma kifungu cha hadithi kilichotolewa; Kufupisha kifungu kwa maneno 110-115; Kusomea mwenzake ufupisho wake ili apate maoni; Kuandika nakala safi ya ufupisho. |
Mbinu zipi zinasaidia kufupisha kifungu kwa kuzingatia idadi ya maneno inayohitajika?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 79
Kifungu cha hadithi Karatasi za kuandikia |
Kufupisha kifungu kwa idadi maalum ya maneno;
Kupangilia habari kwa mtiririko wa maana;
Kuzingatia vipengele vya ufupisho
|
|
6 | 4 |
Kuandika
|
Insha za Kubuni - Maelezo
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya insha za maelezo; Kutambua vipengele vya lugha inayoathiri hisia mbalimbali katika insha za maelezo; Kueleza umuhimu wa kutumia lugha inayoathiri hisia katika insha za maelezo; Kuandika insha ya maelezo akitumia lugha inayoathiri hisia mbalimbali; Kufurahia kutumia lugha inayoathiri hisia katika insha za maelezo. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma kielelezo cha insha ya maelezo; Kudondoa na kuandika mafungu ya maneno yanayogusa hisia; Kutambua jinsi matumizi ya tashbihi, chuku, maswali ya balagha, na ulinganishi wa hali kinzani yalivyoathiri hisia; Kujadili umuhimu wa lugha inayoathiri hisia katika insha. |
Je, ni nini kinafanya maelezo katika insha kudhihirika?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 82
Kielelezo cha insha ya maelezo Kamusi KLB Top Scholar Kiswahili uk. 83 Vifaa vya kidijitali Karatasi za kuandikia |
Kueleza maana ya insha za maelezo;
Kutambua vipengele vya lugha inayoathiri hisia;
Kueleza umuhimu wa lugha inayoathiri hisia katika insha
|
|
7 | 1 |
Sarufi
|
Vielezi vya Mahali
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vielezi vya mahali katika matini; Kueleza matumizi ya vielezi vya mahali; Kutumia vielezi vya mahali ipasavyo katika matini; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya vielezi vya mahali katika matini mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutazama mafungu ya maneno yenye vielezi vya mahali; Kupigia mstari mafungu yanayoeleza mahali ambapo kitendo kinafanyika; Kutambua vielezi vya mahali katika sentensi; Kutunga sentensi akitumia vielezi vya mahali vifuatavyo: shuleni, kwenye soko, Kenya, ndani ya mto, gwarideni, katika gari. |
Vielezi vya mahali huundwaje?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 84
Mafungu ya maneno Chati |
Kutambua vielezi vya mahali;
Kutunga sentensi akitumia vielezi vya mahali;
Kupigia mstari vielezi vya mahali katika kifungu
|
|
7 | 2 |
Sarufi
|
Vielezi vya Idadi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vielezi vya idadi katika matini; Kueleza maana ya vielezi vya idadi; Kutumia vielezi vya idadi ipasavyo katika matini; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya vielezi vya idadi katika matini mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutazama kiwambo cha tarakilishi chenye mafungu ya maneno; Kutambua sentensi zinazoeleza kitendo kimetendwa mara ngapi; Kupigia mstari vielezi vya idadi katika kifungu; Kutumia vielezi vya idadi vifuatavyo: mara mbili, mara nyingi, siku saba, juma moja, mara chache, minara kadhaa. |
Vielezi vya idadi hutumiwa vipi katika sentensi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 85
Kiwambo cha tarakilishi Matini yenye vielezi vya idadi |
Kutambua vielezi vya idadi;
Kutunga sentensi akitumia vielezi vya idadi;
Kupigia mstari vielezi vya idadi katika kifungu
|
|
7 | 3 |
MISUKOSUKO YA KIJAMII
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Uzungumzaji wa Kushawishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya uzungumzaji wa kushawishi; Kubainisha miktadha ya uzungumzaji wa kushawishi; Kutambua vipengele vya uzungumzaji wa kushawishi; Kueleza umuhimu wa vipengele vya uzungumzaji wa kushawishi; Kuchangamkia uzungumzaji wa kushawishi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusikiliza aina mbili za uzungumzaji kutoka kwa mwalimu au video; Kubainisha uzungumzaji ambao ni wa kushawishi; Kueleza maana ya uzungumzaji wa kushawishi; Kutazama picha na kubainisha miktadha ya uzungumzaji wa kushawishi. |
Mzungumzaji anashawishi vipi hadhira yake?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 88
Video ya mzungumzaji Picha za miktadha ya uzungumzaji KLB Top Scholar Kiswahili uk. 89 Kifaa cha kidijitali Jedwali la tathmini |
Kueleza maana ya uzungumzaji wa kushawishi;
Kubainisha miktadha ya uzungumzaji wa kushawishi;
Kueleza umuhimu wa vipengele vya uzungumzaji wa kushawishi
|
|
7 | 4 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya mandhari; Kutambua mandhari katika shairi; Kueleza umuhimu wa mandhari katika shairi; Kuchambua mandhari katika shairi; Kuchangamkia usomaji wa mashairi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutafuta kwenye kamusi au mtandaoni maana ya neno mandhari; Kusoma shairi "Misukosuko ya nini?"; Kutambua mandhari katika shairi, akizingatia mahali matukio yanapotokea na kipindi cha matukio yanayorejelewa; Kueleza umuhimu wa mandhari katika shairi. |
Shairi ni nini?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 91
Kamusi Shairi "Misukosuko ya nini?" |
Kueleza maana ya mandhari;
Kutambua mandhari katika shairi;
Kueleza umuhimu wa mandhari katika shairi
|
|
8 | 1 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya muundo wa shairi; Kutambua vipengele vya muundo wa shairi; Kuchambua muundo wa shairi kwa kutumia vipengele maalum; Kuheshimu maoni ya wengine kuhusu muundo wa shairi; Kufurahia kusoma mashairi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma tena shairi "Misukosuko ya nini?"; Kujibu maswali kuhusiana na idadi ya beti, mishororo, vipande, mizani, vina na mtiririko wa mishororo ya mwisho; Kusoma shairi lingine kutoka katika diwani iliyopendekezwa; Kuchambua shairi kwa kuzingatia mandhari na muundo wa shairi. |
Umewahi kusoma shairi kuhusu nini?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 92
Shairi "Misukosuko ya nini?" Diwani iliyopendekezwa |
Kutambua vipengele vya muundo wa shairi;
Kuchambua muundo wa shairi;
Uwasilishaji wa kazi kwa mwalimu
|
|
8 | 2 |
Kuandika
|
Viakifishi - Mabano
Viakifishi - Kistari Kifupi |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua matumizi ya mabano katika matini; Kueleza matumizi ya mabano; Kutumia mabano ipasavyo katika kuakifisha matini; Kufurahia matumizi yafaayo ya mabano katika matini mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma sentensi zenye mabano; Kueleza matini iliyofungiwa kwa alama za mabano; Kutambua matumizi ya mabano katika sentensi kuonyesha kisawe cha neno, kutoa ufafanuzi wa neno na kufungia nambari katika orodha; Kuakifisha kifungu kwa kutumia mabano. |
Mabano hutumiwa kufanya nini katika kuandika sentensi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 93
Sentensi zenye mabano Kifungu cha kuakifisha KLB Top Scholar Kiswahili uk. 94 Vifungu vyenye kistari kifupi Karatasi za kuandikia |
Kutambua matumizi ya mabano;
Kueleza matumizi ya mabano;
Kutumia mabano ipasavyo kuakifisha
|
|
8 | 3 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua nomino za ngeli ya U-ZI; Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya U-ZI; Kutumia nomino za ngeli ya U-ZI katika matini; Kuheshimu maoni ya wenzake; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya ngeli ya U-ZI katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua nomino za ngeli ya U-ZI katika mnyororo wa nomino; Kusoma sentensi zenye nomino za ngeli ya U-ZI katika jedwali la umoja na wingi; Kutambua kiambishi cha upatanisho wa kisarufi cha ngeli ya U-ZI; Kutunga sentensi katika umoja na wingi akitumia nomino za ngeli ya U-ZI. |
Ni vitu gani katika mazingira yako vyenye majina yaliyo katika ngeli ya U-ZI?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 95
Mnyororo wa nomino Jedwali la sentensi |
Kutambua nomino za ngeli ya U-ZI;
Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi;
Kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya U-ZI
|
|
8 | 4 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua nomino za ngeli ya YA-YA; Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya YA-YA; Kutumia nomino za ngeli ya YA-YA katika matini; Kuheshimu maoni ya wenzake; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya ngeli ya YA-YA katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua nomino za ngeli ya YA-YA katika orodha ya maneno; Kusoma sentensi zenye nomino za ngeli ya YA-YA katika umoja na wingi; Kutambua kiambishi cha upatanisho wa kisarufi cha ngeli ya YA-YA; Kutunga sentensi katika umoja na wingi akitumia nomino za ngeli ya YA-YA. |
Ni vitu gani katika mazingira yako vyenye majina yaliyo katika ngeli ya YA-YA?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 96
Orodha ya nomino za ngeli ya YA-YA Sentensi za umoja na wingi |
Kutambua nomino za ngeli ya YA-YA;
Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi;
Kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya YA-YA
|
|
9 |
Midterm |
||||||||
10 | 1 |
MATUMIZI YA VIFAA VYA KIDIJITALI KATIKA BIASHARA
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kusikiliza kwa Kina - Sauti /j/ na /nj/
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua sauti /j/ na /nj/ katika maneno; Kutamka maneno yenye sauti /j/ na /nj/ ipasavyo; Kutofautisha sauti /j/ na /nj/ kimatamshi; Kuchangamkia matamshi bora ya sauti /j/ na /nj/ katika mazungumzo ya kawaida. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutambua sauti /j/ na /nj/ katika maneno kwenye kapu la maneno; Kunakili maneno aliyoyatambua na kupigia mstari sauti /j/ na /nj/; Kumtamkia mwenzake maneno hayo; Kumtamkia mwenzake maneno mengine anayojua yenye sauti /j/ na /nj/. |
Ni maneno yapi unayoyajua yaliyo na sauti /j/ na /nj/?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 98
Kapu la maneno Ujumbe wa kibiashara KLB Top Scholar Kiswahili uk. 99 Kifaa cha kidijitali Jozi za maneno zenye sauti /j/ na /nj/ |
Kutambua sauti /j/ na /nj/ katika maneno;
Kutamka maneno yenye sauti /j/ na /nj/;
Kutofautisha sauti /j/ na /nj/ kimatamshi
|
|
10 | 2 |
Kusoma
|
Ufahamu wa Kifungu cha Kushawishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kudondoa habari mahususi katika kifungu cha kushawishi; Kueleza maana za maneno kama yalivyotumiwa katika kifungu cha kushawishi; Kutumia msamiati unaotokana na kifungu cha kushawishi ipasavyo; Kuchangamkia usomaji wa kifungu cha kushawishi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma makala kuhusu Lena aliyeanzisha biashara; Kudondoa habari muhimu kutoka kwenye kifungu kwa kujibu maswali; Kueleza maana za maneno yaliyotumika katika kifungu; Kutunga sentensi akitumia maneno hayo. |
Je, unafanya nini ili kupata habari zilizoko katika kifungu cha kushawishi kwa usahihi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 100
Makala ya Lena Kamusi |
Kudondoa habari mahususi;
Kueleza maana za maneno;
Kutumia msamiati unaotokana na kifungu
|
|
10 | 3 |
Kusoma
|
Ufahamu wa Kifungu cha Kushawishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana za maneno kama yalivyotumiwa katika kifungu cha kushawishi; Kutumia msamiati unaotokana na kifungu cha kushawishi ipasavyo; Kutambua lugha shawishi katika kifungu; Kuchangamkia usomaji wa kifungu cha kushawishi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kueleza maana za maneno yafuatayo: "msilaze damu", "ajira", "kupigia debe", "alinasa makini", "imenikimu", "kuchuuza"; Kutunga sentensi akitumia maneno hayo; Sakura katika mtandao kifungu kuhusu matumizi ya vifaa vya kidijitali katika biashara; Kujibu maswali baada ya kusoma kifungu. |
Unawezaje kugundua kuwa mwandishi wa kifungu anajaribu kukushawishi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 101
Jedwali la tathmini Mtandao salama |
Kueleza maana za maneno;
Kutumia maneno katika sentensi;
Kutambua lugha shawishi
|
|
10 | 4 |
Kuandika
|
Insha za Kubuni - Masimulizi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza ukuzaji wa wazo baina ya aya za insha ya masimulizi; Kutambua vipengele vya ukuzaji wa wazo baina ya aya za insha ya masimulizi; Kubainisha vipengele vya ukuzaji wa wazo baina ya aya za insha ya masimulizi; Kupenda kutumia vipengele vya ukuzaji wa wazo baina ya aya za insha ya masimulizi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma mojawapo ya insha za masimulizi zilizohifadhiwa kwenye potifolio; Kueleza mawazo yalivyokuzwa baina ya aya; Kutambua vipengele vya ukuzaji wa wazo katika insha aliyoisoma; Kutambua wazo kuu, maelezo, mifano na hitimisho katika kila aya. |
Je, unafanya nini ili kulikuza wazo baina ya aya za insha ya masimulizi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 103
Insha za masimulizi zilizohifadhiwa Karatasi za kuandikia KLB Top Scholar Kiswahili uk. 104 Vidokezo vya insha |
Kueleza ukuzaji wa wazo baina ya aya;
Kutambua vipengele vya ukuzaji wa wazo;
Kubainisha vipengele vya ukuzaji wa wazo
|
|
11 | 1 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua nomino za ngeli ya LI; Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya LI; Kutumia nomino za ngeli ya LI katika matini; Kuheshimu maoni ya wenzake; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya ngeli ya LI katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kunakili sentensi zenye nomino za ngeli ya LI; Kutambua kiambishi cha upatanisho wa kisarufi katika sentensi alizonakili; Kusoma maneno yaliyo kwenye chati; Kutambua nomino za ngeli ya LI katika maneno yaliyo kwenye chati; Kutumia nomino za ngeli ya LI kutunga sentensi. |
Ni vitu gani katika mazingira yako vyenye majina yaliyo katika ngeli ya LI?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 105
Sentensi zenye nomino za ngeli ya LI Chati ya maneno |
Kutambua nomino za ngeli ya LI;
Kutambua kiambishi cha upatanisho wa kisarufi;
Kutumia nomino za ngeli ya LI kutunga sentensi
|
|
11 | 2 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua nomino za ngeli ya KU na PA-KU-MU; Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KU na PA-KU-MU; Kutumia nomino za ngeli ya KU na PA-KU-MU katika matini; Kuchangamkia matumizi yafaayo ya ngeli ya KU na PA-KU-MU katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kunakili sentensi zenye nomino za ngeli ya KU; Kutambua viambishi vya upatanisho wa ngeli ya KU kwa kuvipigia mstari; Kusoma nomino kwenye kadi; Kutambua nomino za ngeli ya KU kutoka kwenye kadi; Kutumia nomino katika ngeli ya KU kutunga sentensi; Nakili sentensi zenye viambishi vya ngeli ya PA-KU-MU. |
Je, viambishi vya ngeli ya PA-KU-MU vinatofautiana vipi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili uk. 106
Sentensi zenye nomino za ngeli ya KU Kadi za nomino Sentensi zenye viambishi vya ngeli ya PA-KU-MU |
Kutambua nomino za ngeli ya KU na PA-KU-MU;
Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi;
Kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya KU na PA-KU-MU
|
|
11 | 3 |
KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Mazungumzo - Malumbano ya Utani
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya malumbano ya utani. Kueleza mambo yanayosimuliwa katika malumbano ya utani. Kutambua vipengele vya uwasilishaji wa malumbano ya utani. Kuchangamkia kuwasilisha malumbano ya utani kwa kutumia vipengele vya kimsingi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kuonyeshwa picha ya watu wanaowasiliana kisha aeleze wanafanya nini. Kuigiza malumbano ya utani yaliyotolewa kielelezo na mwalimu. Kutambua maneno yanayoonyesha mzaha. Kushiriki majadiliano ya kikundi kuhusu maana ya malumbano ya utani kwa kurejelea mfano uliogizwa. |
Je, unajua malumbano ya utani ni nini?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 108
Picha Maigizo ya malumbano ya utani Kifaa cha kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 109 Chati ya vipengele vya uwasilishaji wa malumbano ya utani |
Kueleza maana ya malumbano ya utani
Kutambua vipengele vya malumbano ya utani
Kuigiza malumbano ya utani
|
|
11 | 4 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya wahusika katika fasihi. Kutambua wahusika katika shairi. Kujadili sifa za wahusika katika shairi. Kuchangamkia kutambua wahusika katika mashairi mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kutaja majina ya watu katika novela au tamthilia alizosoma. Kueleza maana ya wahusika. Kusoma shairi "Uwele huu ni gani?" ukurasa wa 110. Kutambua wahusika katika shairi alilosoma kwa kujibu maswali. |
Je, wahusika ni nani katika kazi ya fasihi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 110
Diwani ya mashairi Kamusi Vifaa vya kidijitali |
Kueleza maana ya wahusika katika fasihi
Kutambua wahusika katika shairi
Kujadili sifa za wahusika katika shairi
|
|
12 | 1 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Ushairi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua wahusika katika shairi. Kujadili sifa za wahusika katika shairi. Kuchambua wahusika katika shairi. Kuchangamkia kutambua wahusika katika mashairi mbalimbali. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma tena shairi "Uwele huu ni gani?" Kujadili sifa za wahusika. Kutambua hisia, tabia, na matendo ya wahusika. Kusoma diwani ya mashairi iliyopendekezwa na mwalimu. Kuchambua shairi moja kwa kuzingatia sifa za wahusika. |
Je, ni vigezo gani vinatumika kutambua wahusika katika shairi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 111-112
Diwani ya mashairi Chati ya sifa za wahusika Kifaa cha kidijitali |
Kutambua wahusika katika shairi
Kujadili sifa za wahusika katika shairi
Kuchambua shairi kutoka kwenye diwani
|
|
12 | 2 |
Kuandika
|
Barua ya Kuomba Kazi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya barua rasmi ya kuomba kazi. Kutambua vipengele vya barua rasmi ya kuomba kazi. Kujadili lugha inayofaa katika kuandika barua rasmi ya kuomba kazi. Kuchangamkia kuandika barua rasmi ya kuomba kazi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kusoma barua rasmi ya kuomba kazi ya Paulo Mwakazi iliyoko kwenye kitabu. Kueleza maana ya barua rasmi ya kuomba kazi. Kutambua vipengele vya barua rasmi ya kuomba kazi. Kujadili lugha inayofaa katika kuandika barua rasmi ya kuomba kazi. |
Je, barua rasmi ya kuomba kazi ina sifa gani?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 113
Kielelezo cha barua rasmi ya kuomba kazi Chati ya vipengele vya barua rasmi Kifaa cha kidijitali KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 114 Kielelezo cha barua ya kuomba kazi Orodha ya vipengele vya barua rasmi |
Kueleza maana ya barua rasmi ya kuomba kazi
Kutambua vipengele vya barua rasmi ya kuomba kazi
Kueleza lugha inayofaa katika barua rasmi ya kuomba kazi
|
|
12 | 3 |
Sarufi
|
Vinyume vya Vihusishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kueleza maana ya vinyume vya vihusishi. Kutambua vinyume vya vihusishi katika matini. Kutumia vinyume vya vihusishi katika sentensi. Kufurahia kutunga sentensi zenye vinyume vya vihusishi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kulinganisha picha za A na B. Kujadili na mwenzake uhusiano wa vitu katika picha za A na B. Kueleza maana ya vinyume vya vihusishi. Kutambua kihusishi na kinyume chake katika jedwali lililotolewa. |
Je, vinyume vya vihusishi vinatumikaje katika sentensi?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 115
Picha Chati ya vihusishi na vinyume vyake Majedwali |
Kueleza maana ya vinyume vya vihusishi
Kutambua vihusishi na vinyume vyake
Kuandika vihusishi na vinyume vyake
|
|
12 | 4 |
Sarufi
|
Vinyume vya Vihusishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo, Kutambua vinyume vya vihusishi katika matini. Kutumia vinyume vya vihusishi ipasavyo katika sentensi. Kutunga sentensi zenye vinyume vya vihusishi. Kuchangamkia matumizi ya vinyume vya vihusishi katika mawasiliano ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
Kupigia mstari vihusishi na vinyume vyake katika sentensi zilizotolewa. Kusoma kifungu na kutambua vihusishi na vinyume vyake. Kujaza nafasi kwenye kifungu kwa kutumia kinyume cha kihusishi kilichotolewa kwenye mabano. Kutunga sentensi akitumia vinyume vya vihusishi vilivyotajwa. |
Je, ni vipi tunaweza kutofautisha vihusishi na vinyume vyake?
|
KLB Top Scholar Kiswahili Gredi ya 9 uk. 116-117
Vifaa vya kidijitali Orodha ya vihusishi na vinyume vyake Kifungu cha ufahamu |
Kutambua vihusishi na vinyume vyake katika kifungu
Kujaza pengo kwa vinyume vya vihusishi
Kutunga sentensi zenye vinyume vya vihusishi
|
Your Name Comes Here